
Katika kesi aliyoifungua Hilda na kusikilizwa hukumu kutolewa Jumatano iliyopita, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Temeke, Kassim Sapi Mkwawa aliamuru mwili wa Emmanuel uzikwe katika shamba la mjomba wa marehemu Dk. Mercezederc Nambuo Temu ambaye ni kiongozi wa ukoo katika Kijiji cha Kitahie, mkoani Kilimanjaro. Awali kesi hiyo ya madai namba saba ya mwaka 2014, ilifunguliwa mahakamani hapo na Hilda Lewi Nambuo Temu, ambaye ni mama mzazi wa marehemu, akitaka mazishi ya mwanaye Emmanuel yafanyike Kijiji cha Kitahie Old Moshi mkoani Kilimanjaro lakini Jacob alipinga. Hakimu Mkwawa wakati wa kutoa hukumu hiyo alisema:
“Baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili nimebaini kuwa pande zote mbili za ndugu wanachobishana si Kijiji cha Kitarara wala Kitahie bali hawataki marehemu azikwe kwenye shamba la ukoo. “Lakini kwa kuwa baba mkubwa wa marehemu Dk Mercezederc amekubali marehemu Emmanuel azikwe kando ya shamba lake lililopo Kitahie, hakuna aliyepoteza baina ya pande zote mbili, hivyo marehemu akazikwe hapo,” alisema hakimu na akasema gharama za kesi kila upande ujibebee. Kutokana na hukumu hiyo, marehemu Emmanuel anatarajiwa kuzikwa katika Kijiji cha Kitahie Old Moshi mkoani Kililimanjaro Machi 8, mwaka huu (leo), baada ya kukaa mochwari kwa siku 20.
0 comments:
Post a Comment