MAAJABU! Licha ya ulimwengu wa burudani Bongo kuamini kwamba staa wa
Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliwahi kuanguka dhambini kwa
Mbongo-Fleva, Elias Barnaba, mwanadashosti huyo ameibuka na kudai kuwa
hakuwahi kumpa penzi.
Shilole akifanya mahojiano na Global TV Online.
Shilole anayetamba na Ngoma ya Nakomaa na Jiji, amefunguka hayo
kupitia Global TV Online ambapo mahojiano hayo yatarushwa kwenye Mtandao
wa Global leo, Jumatatu. “Ukweli sikumpa penzi Barnaba, yule ni mshkaji tu…kama ni muziki
hakunipiga tafu kama alivyonisaidia Q-Chillah …hahaha acha hizo bwana,
Barnaba hakuwa mchumba wangu,” alisema Shilole.
Elias Barnaba.
Mbali na kumfungukia Barnaba kwenye kipindi hicho, Shilole amefunguka mambo mengi ambayo hajawahi kuyasema.
0 comments:
Post a Comment