MWANADADA anayefanya
vizuri katika kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema
watoto wanamkumbusha namna alivyoishi akiwa yatima, hivyo anawapenda
sana.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Nisha alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar
juzikati wakati wa hitima ya kuwakumbuka marehemu ambapo Nisha
alionekana kuwa kivutio kwa watoto waliofika viwanjani hapo kwa ajili ya
kaswida, kwani mara baada ya kisomo kumalizika, watoto hao walimfuata
na kucheza naye.
“Kiukweli, nimefurahi sana kucheza nao kwani watoto ndiyo watu pekee
wanaonipa furaha katika maisha yangu kwani mimi ni mtoto yatima,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment