MSANII wa filamu Bongo, Jimmy Mafufu amewabwatukia mastaa wenye tabia
za chuki za kuwaroga wenzao na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Jimmy Mafufu.
Akichonga na paparazi wetu, Mafufu alisema anashangazwa jinsi wasanii
wasivyopenda mafanikio ya wengine wakati usanii hauna uhusiano wowote
na chuki, fitna na majungu. “Hii ni roho mbaya na ya kishetani, yaani wasanii wengi wamejiingiza
kwenye vitendo vya kishirikina ili kuwaumiza wengine, tasnia imejaa
majungu, wasisahau Mungu yupo na anaona,” alisema Mafufu.
0 comments:
Post a Comment