Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya.
Akizungumza na mapaparazi wetu katikati ya wiki hii ofisini kwake
Magomeni-Mwembechai jijini Dar, Maalim alitumia saa kadhaa kuangalia
nyota ya mmoja baada ya mwingine na kueleza sifa zao katika sekta ya
uhusiano na tendo la ndoa.
ALIANZA NA WEMA
Akimzungumzia Wema aliyezaliwa Septemba 28, Maalim alisema nyota yake ni Mizani hivyo ana tabia zifuatazo katika masuala ya mapenzi:
“Kwanza yeye (Wema) na Diamond nyota yao ni moja hivyo mambo yao mengi yanafanana.
“Wanapenda kuwa kwenye ulimwengu wa mapenzi na mahaba wakati wote. Wanathamini sana masuala ya ngono kuliko maisha mengine.”

“Hawa watakuwa watu wa kuachana na kurudiana mpaka watakapofunga ndoa ya kifahari hapo baadaye.
“Kuhusu mambo mengine kinyota ni kwamba wana sifa ya uongozi, wanapenda kuwa huru na kujitegemea. Wanapenda kuheshimika kwenye jamii na ni wacheshi, wana hekima na diplomasia.”

Kwa upande wake Ray ambaye amezaliwa Mei 28, Maalim alisema nyota yake ni Mapacha.
Akimchambua kinyota kuhusu masuala ya mapenzi, alisema:
“Akimpenda mwanamke ana uwezo wa kumpa chochote, kimawazo na kila kitu, anaweza hata kuhamia nyumbani kwa mwanamke huyo.

“Pia anapenda kuwa na mapenzi ya siri siku zote. Hata akioa ni lazima ataendelea kuwa na mwanamke wa nje ‘nyumba ndogo’.
“Mbali na masuala hayo, ni mtu mwenye hisia kali sana ambapo hukasirika upesi. Ni mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kuzungumza, ana ushawishi mbele za watu.”

Akimchambua Aunt Ezekiel ambaye alizaliwa Oktoba 27, mtabiri huyo alisema nyota yake ni Nge.
“Kinyota, ni mtu mwenye ‘muwashawasha’ wa mapenzi, anapokuwa na hasira tu hupenda kuzimaliza kwa kufanya tendo la ndoa.
“Ni msiri sana. Ana wapenzi wengi lakini kwa siri. Kwake tendo la ndoa ni ishu muhimu sana katika maisha yake hasa ikizingatiwa kuwa, nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.
“Kwa mwenye moyo mdogo, asifanye mapenzi na mtu mwenye nyota hii kwani atajuta maisha yake yote. Lakini hayumbi na hakubali kushindwa hata kwa jambo ambalo halitamharibia popote.”

Kwa upande wa JB aliyezaliwa Desemba 4, Wolper aliyezaliwa Desemba 6, Maalim alisema wote wana nyota moja inayofanana ya Mshale. Anaichambua nyota hiyo hivi:
“Wanapenda kufanya ngono kwa muda mrefu, hivyo mwanamke au mwanaume atakayekuwa nao kimapenzi lazima awe amekula akashiba vizuri kabla ya tendo lenyewe.

“Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu na wanakolea vilivyo. Mara nyingi wanapenda sana kuwa na wapenzi wapya, lakini hawapendi mapenzi ya kudumu kwa sababu yanawanyima uhuru.

Akimzungumzia Johari aliyezaliwa Agosti Mosi, mtaalam huyo alisema nyota yake ni Simba. Anasema:
“Kinyota ana tatizo la kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani ni mtu anayeumia.
“Mara nyingi hujipa hisia za kupendwa na mpenzi wake kama anavyompenda yeye.
“Ni mkarimu lakini ni jeuri, anapenda sana kuonea wenzake. Anapenda kujionesha na humharibu mpenzi wake.”
0 comments:
Post a Comment